BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Friday, April 19, 2013

AUNT:WABUNGE WANATAKA KUNIVUNJIA NDOA

DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake, Amani linasimulia aliyoyasema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.

“Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza: “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.” Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte, Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...